Jumapili 8 Februari 2026 - 21:30
Israel inataka kuanzisha vita vya ndani nchini Lebanon

Hawza/ Ali Fayyadh alisisitiza kwamba; Lebanon iko katika hatua nyeti na ya hatima, inayowataka wananchi wote watende kwa kiwango cha juu cha uwajibikaji ili tuweze kuiokoa Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ali Fayyadh, mbunge wa Lebanon na mjumbe wa kambi ya Uaminifu kwa Muqawama, katika mkutano wa kisiasa uliofanyika katika Kituo cha Imam Khomeini (r.a.) kilichopo Tahwitat al-Ghadir, kwa huku wakazi wa mji wa Blida wakishiriki, alisisitiza kuwa; nchi iko katika hatua nyeti na ya hatima inayowataka watu wote watende kwa kiwango cha juu cha uwajibikaji ili kuiokoa Lebanon, kuifikisha kwenye usalama, na kusimama imara mbele ya mashinikizo na changamoto nyingi. Jambo hili linahitaji mazungumzo, mashauriano na maelewano kuhusu masuala muhimu na ya hatima yanayoikabili nchi.

Aliongeza kuwa; katika hatua hii kuna shinikizo la wazi na linaloonekana, hasa katika juhudi za kugeuza eneo la kaskazini mwa Mto Litani kuwa uwanja wa kuongezeka kwa mvutano na migogoro kati ya jeshi la Lebanon, muqawama na mazingira yake ya kijamii.

Fayyadh alisema: Tunaamini na tuna uhakika kwamba; uongozi wa jeshi la Lebanon una hekima, hisia ya uwajibikaji wa kitaifa na uelewa wa kutosha wa kushughulikia hatua hii kwa kiwango cha juu cha ukomavu, maendeleo na busara; kwa sababu jeshi la Lebanon ni jeshi letu la kitaifa, maafisa na askari wake ni watoto wetu, na sisi ni familia yao. Bila shaka tutakabiliana na hatua hii kwa namna ambayo adui hataweza kufikia malengo yake.

Mjumne huyo wa kambi ya muqawama alisisitiza kuwa; muqawama hauna dalili yoyote ya silaha si kaskazini mwa Mto Litani wala katika maeneo mengine, na haufanyi shughuli yoyote ya kijeshi inayokwenda kinyume na mamlaka ya dola au harakati za uwanjani na jukumu la jeshi la Lebanon. Kwa hiyo aliwataka wote kuwa waangalifu kuhusu hatari zilizopo nchini, na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo, mawasiliano na mashauriano, ili adui asibadilishe asili ya mzozo kutoka suala kati ya Lebanon na utawala wa Kizayuni kuwa suala kati ya Walebanon wenyewe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha